HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 23 February 2018

JAMII YAASWA KULIANGALIA KWA UZITO SUALA LA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

Na Anil Ricco, Globu ya Jamii
Jamii ya Kitanzania imeaswa kuliangalia kinaga ubaga suala la nafasi ya uongozi katika jamii kwa kulijadili suala hilo mara kwa mara.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Wanachama wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wameomba  Sheria ya Vyama vya Siasa itungwe katika uwiano wa kijinsia ili kuwapa nafasi katika Uongozi.

Mjumbe wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Bi. Leticia Mkulasi amesema kuwa sio vizuri kujadili suala hilo mpaka zinaposimama Chaguzi, bali kuna umuhimu wakuhamasisha jamii mara kwa mara.

Pia amesema anaamini Waandishi wa Habari wanaweza kutoa taarifa zitakazo elimisha jamii juu ya nafasi ya Mwanamke katika Uongozi na masuala ya kisiasa kwa ujumla.

Naye Mwanachama wa Mtandao wa ULINGO, Bi. Maria Kigalu amesema Msajili wa Vyama vya Siasa yuko katika mchakato wakuchakata Sheria mpya ya Vyama vya Siasa, hivyo anaamini itasaidia Wanawake kupata nafasi ya uongozi wa siasa.

Amesema Mchakato wa mwaka huu wa Sheria ya Vyama vya Siasa utakaojadiliwa Bungeni utakuwa tofauti na mchakato wa mwaka 2013 ambao haukufanyiwa kazi kipengele cha nafasi ya Mwanamke katika Uongozi.
Mmoja wa Watoa Maada katika Mkutano huo, Dkt. Dina Mbaga akielekeza jambo kwa baadhi ya Waandishi wa Habari na Wanachama wa Mitandao mbalimbali waliohudhulia Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwanachama wa Woman Fund Tanzania (WFT), Bi. Leticia Mkulasi akitoa mada kwa Waandishi wa Habari na baadhi ya Wanachama wa Mitandao mbalimbali ya Wanawake nchini kuhusiana na Suala la nafasi ya Mwanamke katika Uongozi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad