HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 12, 2018

HALMASHAURI HANANG YASHAURIWA KUANZISHA CHANZO KIPYA CHA UTALII WA MLIMA HANANG

Na Jumbe Ismailly -HANANG
PAMOJA na serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini wazazi na walezi wa wanafunzi katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang bado wamekuwa kikwazo cha watoto wao kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Brycosen Kibassa aliyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na kituo hiki alipokuwa akizungumzia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya hiyo kutokana na wazazi au walezi kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani yao ya kumaliza masomo yao.

Aidha Mkurugenzi huyo aliweka bayana kwamba mwaka 2017 Halmashauri hiyo iliweka mpango na wakakubaliana kwamba kiwango cha ufaulu kwa wastani uwe asilimia 80 kwa wilaya na licha ya kufanya majaribio mengi kabla ya kufikia mtihani wa taifa,ambapo katika mtihani wa majaribio walipata wastani wa asilimia 75.

Kwa mujibu wa Kibassa baada ya kufanya mtihani huo wa kitaifa wamepata asilimia sita hali ambayo ni dhahiri kwamba iliwashitua sana na kuanza kuangalia kilichosababisha hali hiyo na katika taarifa za awali walizonano inaonekana wazazi wenye mwamko mdogo wa elimu katika eneo hilo waliwatuma kwa makusudi kabisa watoto wao kwamba wahakikishe hawafanyi vizuri katika mitihani yao.

Akizungumzia mikakati waliyojipanga kukabiliana na hali hiyo,Kibassa pamoja na kukiri kwamba kuna baadhi ya maeneo ya usimamizi kwa upande wa ngazi ya wilaya hawakuwa wamejipanga vizuri sana na kutolea mfano kitengo cha udhibiti ubora wa elimu ambacho kinahusika na ukaguzi wa elimu kuwa kwa mwaka huu watafanya kazi kama timu kuanzia idara ya elimu,wadau wa elimu sambamba na kuwatumia maafisa elimu kata kuhakikisha wanasimamia kwa karibu kwenye maeneo yao.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wakizungumzia changamoto hiyo,Mary Gwau aliwashauri wazazi kuona umuhimu wa elimu kwani ni maisha kwa watoto wao na kwamba mtu anapokuwa na elimu huweza kujisaidia katika maisha yake na anaweza kuwa mtu wa maana katika siku za baadaye na ataweza kuwasaidia wazazi wake.

“Hivyo kama wazazi tuchukue jukumu la kuwasogelea watoto wetu na kupata elimu kwamba tuwasaidie hawa watoto wasome wapate elimu ili nao wajiwezeshe tusijiunge na yale makundi ya watu ambao wamekata tamaa,kusomesha watoto hawataki kuwatia moyo hawataki kabisa”alisisitiza Mzazi huyo.

Naye Mzazi Eliasi Kaila aliwatahadharisha wazazi na walezi wa wanafunzi kutokuwa chanzo cha kukwamisha elimu kwa watoto wao na badala yake wawe chachu ya watoto kupata elimu na kushauri kwamba wajenge utamaduni wa kuwafundisha nyumbani badala ya kuwategemea walimu peke yao.

“Mzazi asiwe chanzo cha kumkwamisha mtoto kupata elimu kwa sababu hivi sasa elimu ni bila malipo na rais mwenyewe amesema na mwananchi asichangishwe mchango wa aina yeyote kuhusu mtoto wa shule”.alifafanua Kaila.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara wakiwa wamesimama kwa muda wa takribani dakika tano kuashiria kumkumbuka mmoja wa madiwani hao aliyepoteza maisha katika siku za hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nangwa waliohudhuria mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo wasikiliza kinachojadiliwa na wawakilishi wao waliowachagua.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,CharlES Yona akisisitiza juu ya umuhimu wa kudumisha ushirikiano katika utendaji wa shughuli zote za Halmashauri ya Hanang,lengo likiwa ni kuisogeza mbele kimaendeleo Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Bryceson Kibassa (wa kwanza kulia) akimpongeza diwani wa kata ya Nangwa,Portagia Baynet muda mfupi baada ya kuapisha na kula kiapo cha uadilifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad