HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 27 February 2018

AZAM FC, SINGIDA UNITED KUKIPIGA JUMAMOSI HII

Na Agness Francis Globu ya jamii 

MABINGWA wa Afrika Mashariki na kati AzamFc wanatarajiwa  kukutana tena na Singida United kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara. Mtanange huo utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi  siku ya Jumamosi ya wiki hii ,saa 10 jioni huku Azam akiwa wenyeji wa Singinda united. 

Ambapo Singida  tangu kupanda daraja msimu huu hawajawahi kucheza na mabingwa hao katika  uwanja huo. 

Akizungumza leo katika ofisi zao Mzizima Jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa AzamFc  Jaffary Iddy Maganga  amesema katika raundi iliyopita timu hizo mbili zilitoka sare kwa kufungana 1-1 katika Uwanja wa  Jamuhuri Dodoma.

Wakati Singinda United walipokuwa wakiuchezea uwanja huo kama wa nyumbani kabla wa kwao kukamilika. 

Jaffary amesema kikosi cha Azam jana kimeingia kambini na kuanza mazoezi ya kujifua ili kukabiliana na Timu hiyo. 

"Tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Singinda Timu yao ni ya ushindani na imeonyesha ujasiri wa hali ya juu kutokana na jinsi Kikosi chao walivyokisajili,"amesema Maganga. 

Hata hivyo Maganga amesema licha ya kukabiliwa na mchezo huo mgumu wataakikisha pointi 3 zinabaki Nyumbani. 

"Wachezaji wetu,  Himidi Mau pamoja na Waziri Junior  tayari wamerejea kikosini kwa ajili ya mazoezi na itategemea mpaka kufikia Jumamosi,  Mwalimu ataamua Wachezaji  hao wacheze  mchezo au lah kutokana na unafuu wao utakavyokuwa," amesema Maganga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad