HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 8, 2018

WAZIRI MPINA AKAMATA KILO 65,600 ZA SAMAKI ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA TATU

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (katikati )akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bi Mwanaidi Mlolwa akitoa maelezo baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 jijini Bukoba waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba leo.Mwenye koti ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyenyanyua mikono ) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (mwenye koti) leo, nje ya ghala la kuhifadhia samaki katika ofisi ya Uvuvi jijini Bukoba mara baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (aliyesimama) akisoma taarifa ya mkoa kuhusu sekta ya mifugo na Uvuvi kwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (alikaa kulia kwake) leo, mara baada ya kufanya ziara ya ghafla leo ili kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi nchini, Mwanaidi Mlolwa.
Sehemu ya shehena ya samaki wachanga waliokaushwa kwa chumvi aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba, wakiwa wamehifadhiwa katika ghala kwenye ofisi ya Uvuvi jijini Bukoba. Samaki hao walikaatwa kufuatia raia mwema kutoa taarifa kwa Waziri Luhaga Mpina hivi karibuni.

Mwandishi Maalum, Bukoba

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.

Waziri Mpina alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya usalama kwa mlaji na kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.

Aidha Waziri aliongeza kwamba Sheria hiyo imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) pamoja na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 29 ya mwaka 1994.

Waziri Mpina ameagiza watendaji kufuata taratibu zote za kisheria ili samaki hao wauzwe kwa njia ya mnada na mapato hayo yaingie Serikalini mara moja.Aidha aliwaonya wafanyabiashara na wavuvi kuachana na uvuvi haramu kwa kuwa ni kuhujumu raslimali za taifa ambazo zingetumika kwa kizazi cha sasa na baadaye.

“Mfanyabiashara yoyote wa samaki na mazao yake anayetaka kufilisika na kutafuta matatizo katika maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu”alisisitiza Mpina

Kufuatia tukio hili, Waziri Mpina amewapa wiki mbili wafanyabiashara na wasafirishaji wote wa samaki na mazao yake waliopewa leseni ya ya kufanya biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji kodi ambapo amesema kama watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo.

Alisema kuanzia sasa wafanyabiashara wote wote wataruhusiwa kupata leseni hiyo baada ya kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa ulipaji kodi, cheti cha usajili wa kampuni na mahesabu ya kibiashara yaliyohakikiwa ili kuepuka utaratibu wa sasa ambao unatoa mwanya kwa mawakala wa ndani na nje ya nchi kujiingiza katika biashara hiyo kinyemela na kuikosesha Serikali mapato kwa kukwepa kulipa kodi mbalimbali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu alisema Serikali itahakikisha kwamba uvuvi haramu unakuwa historia katika Mkoa wa Kagera na kuwataka wananchi kuwafichua wavuvi haramu ili vyombo vya Serikali viwakamate na kuwafikisha katika mikondo ya sheria.

Alisema sekta ya uvuvi inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua hali ya uchumi kwenye mkoa wake na taifa kwa ujumla kama wadau wote watashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo alisema jumla ya wananchi 26,272 wameajiriwa kutokana na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.

Alisema mkoa utaendelea na kupambana na uvuvi haramu ambapo kwa mwaka 2016/17 jumla ya doria 65 zilifanyika na kuwezesha kukamatwa kwa makokoro ya Sangara 422, nyavu ndogo za dagaa 57,nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, ndoano 711, katuli 16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa 86.

Hata hivyo Mkuu huyo alisema katika kuongeza uzalishaji wa samaki jumla ya mabwawa 584 yamechimbwa kwa mwaka 2016/2017 kutoka mabwawa 181 mwaka 2005/2006 sawa na ongezeko la mabwawa 403.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alisema hivi karibuni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.

Alisema Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma na dereva wa gari hilo Ayoub Sanga walishikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= ambapo Ngoma ameshasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Pia Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Mwanaidi Mlolwa alisema Serikali ina mkono mrefu na kwamba hakuna mtu atakayebaki salama iwapo atajihusisha na uvuvi haramu.

Aidha alisema maafisa uvuvi wanawajibu wa kuhifadhi na kutunza takwimu mbalimbali za sekta ya uvuvi ili kutoa picha halisi ya jinsi sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Kimsingi sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad