HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 18, 2018

WAJUMBE BARAZA VYAMA VYA SIASA WAJADILI MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA SHERIA MPYA

Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limekutana na wajumbe wanaounda baraza hilo kwa lengo la kujadili mapendekezo  ya kutungwa kwa ya sheria mpya ya vyama vya siasa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa baraza hilo, John Shibuda amesema katika kujadili mapendekezo mjadala utaanzia katika kamati ya Baraza vyama vya siasa ‘Kamati ya sheria na Utawala Bora’ inaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Hassan Almas na Makamu Mwenyekiti, Sudd Said Sudd.

Amefafanua Kamati ya Sheria na utawala bora itapokea  mpango kitita katoka katika mawazo ya wanachama wa baraza hilo na kuongeza kuwa mchakato wa kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa haujatendeka pamoja mchakato wa mapendekezo  ya sheria usajili wa vyama vya siasa.

Shibuda amesema baraza hilo liko huru bila kusukwa na mtu yeoyote.Amesema ndani ya wiki mbili inatakiwa kamati ya sheria na utawala bora iwe imekamilisha na baada ya hapo wiki mbili zingine iwe ni kwenda kamati ya baraza la vyama siasa inayoongozwa na Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda (pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cho cha baraza la vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Philip Mangula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha vyama vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakifatilia ajenda katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad