HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 19 January 2018

SETHI ASUBIRI MADAKTARI KUTOKA AFRIKA KUSINI KWA UPASUAJI, RUGEMALIRA HANA KANSA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MMILIKI wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi na Mfanyabiashara, James Rugemarila wameomba madaktari wao kutoka India na Afrika kusini kuwepo wakati wakifanyiwa uchunguzi wa afya zao.

Maombi ya mshtakiwa, Harbinder Seth yamewasilishwa na Wakili wake, Alex Balomi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupata taarifa kutoka upande wa mashtaka.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai kuwa alikwenda magereza kufuatilia hali za washitakiwa hao kama mahakama ilivyoagiza.

Swai amedai kuwa washitakiwa hao wameomba magereza wakati wanapofanyiwa uchunguzi kiafya madaktari wao kutoka nje ya nchi wawepo. 

Amesema, mshtakiwa Sethi ambaye anaishi na puto tumboni ambalo kwa uchunguzi aliofanyiwa na daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Desemba mwaka jana linatakiwa litolewe na, mshitakiwa alishirikishwa katika hatua hiyo lakini akaomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati wa kufanyiwa upasuaji.

Aisha amedai mshtakiwa huyo ameomba muda Wa kuwasiliana na daktari wake

Aidha amedai kuwa madaktari wa hapa nchini wamekubaliana na ombi la mshtakiwa ila wamesema kama afya ya mshitakiwa itaendelea kuathirika wataliondoa hilo puto.

Aliendelea kudai, kuhusu afya ya mshtakiwa Rugemalira, yeye anatibiwa na magereza pamoja na daktari wake anayeitwa Fred kutoka Hospitali ya Sanitas ambaye anachukua vipimo na kupeleka hospitalini kwake kisha kurudisha majibu magereza.

Alidai katika majibu hayo yanaonesha kuwa hana saratani kama alivyodai na kwamba serikali inafuatilia afya zao kwani hakuna jambo nyeti litakaloweza kuhatarisha maisha yao.
Wakili Balomi, akipinga hayo amedai, Hospitali ya Muhimbili wamethibitisha kuwa hawana uwezo wa kumfanyia upasuaji wa ama kuondoa au kuweka hilo puto na kusisitiza kwamba umuhimu wa daktari wake kutoka Afrika Kusini ni la kutiliwa mkazo kwani wamepokea maoni kutoka kwa madaktari hao Ka kusisitiza lazima wawepo wakati wa upasuaji.

Naye wakili Respicious Didas wa mshtakiwa Rugemalira amedai ugonjwa wa mteja wake uko wazi kuwa anauvimbe tumboni unaoonekana na upande wa mashtaka hawajachukua hatua yoyote.
Amesema mwaka 2008 mteja wake aliwahi kuugua Kansa na kufanyiwa upasuaji, "kugundulika na matibabu ya kansa yalifanyika nchini India baada ya vipimo vya hapa nchini kumpa shida kugundua tatizo lake.
Amedai anaamini mteja wake akipatiwa matibabu na madaktari wake Wa India wanaweza kugundua tatizo.

Hakimu Simba amesema, mahakama imenukuhu kuwa madaktari wa mshtakiwa wa Seth wawepo wakati wa upasuaji na kusema utaratibu huo huo utumike kwa mshtakiwa Rugemalira, (madaktari wa Magereza wawasiliane na wale wa Muhimbili ili waone umuhimu wa madaktari wake kutoka India wawepo wakati akifanyiwa matibabu).

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashitaka  12 ya  uhujumu uchumi, utakatishaji fedha  na kuisababisha serikali hasara ya  dola za Marekani  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad