HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 21 January 2018

Serikali yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) msimamo wa serikali kwa Klabu ya Michezo ya Simba kuhusu suala la uwekezaji kwa vyama vya michezo vilivyoanzishwa na wanachama kwa kuzingatia wa sheria kuwa ni 49% kwa mwekezaji na 51%  kwa wanachama kufuatia kutangaza kumpa mwekezaji wao 50% hivi karibuni kinyume na kanuni jana jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Salim Abdallah na Katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw. Salim Abdallah akieleza  waandishi habari (hawapo pichani) kuwa msimamo wa serikali wameuelewa na watakwenda kuzungumza na mwekezaji wao Mohamed Dewji kuhusu kumpunguzia 1%  na kumpa 49% badala ya 50% waliyokuwa wametangaza hivi karibuni kumpa jana jijini Dar es Salaam,bpembeni yake ni Mwanasheria wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Evodius Mtawala.

Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali imetoa msisitizo kwa Klabu ya Mchezo ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51% na mwekezaji anachukua 49%.
Msisitizo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw.Mohamed Dewji waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.
“Kanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba  2017 kwa ambapo ilioneka ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata muwekezaji basi mwekezaji achukue 49% na wanachama kutoka na mchango wao kwa mkubwa kwa klabu hiyo basi wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Mheshimiwa Mwakyembe alisema kuwa serikali ya awamu ya tano hajaja kuuwa michezo bali lengo lake ni kuboresha michezo na kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hiyo.
Naye Katibu wa Baraza la Michezo Taifa Bw.Mohamed Kiganga alieleza kuwa ofisi yake ipo katika maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba ya wapamsisitizo wa Serikali katika kuzingatia sheria katika suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki ijayo. 
Kwa Upande wa Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Bw.Salim Abdallah alieleza vyombo vya habari kuwa wanashukuru serikali kwa kuwaeleza kuwa milango iko wazi pale watakapo kuwa na tatizo au watakapo hitaji ushauri wanaweza kuonana na watendaji wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad