HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 5, 2018

KOZI YA MULTI MEDIA ITASAIDIA KUONGEZA UFANISI KWA WAANDAAJI FILAMU NCHINI-WAZIRI MWAKYEMBE

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeahidi kuwasaidia wanafunzi wanasoma kozi ya Multi Media kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo katika sehemu mbalimbali pale inapowawia vigumu kupata nafasi hizo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa lengo la kufahamu  kozi ya Multi Media inayotolewa na chuo hicho namna gani inaweza kusaidia  uandaaji wa filamu nchini.
‘’Kozi hii ya Multi Media ni moja ya masomo yanaweza kuisaidia sekta ya filamu kupata taswira mpya tofauti na ilivyosasa kwani wataalamu hawa wakitumiwa vizuri katika kuandaa filamu  za hapa nchini wanaweza kuleta mabadiliko kwani kwa sasa sekta hiyo ina changamoto kubwa ya kukosa waandaji wenye weledi’’Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Dkt.Mwakyembe aliwapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kuonyesha weledi pale walipokuwa wakijibu  maswali waliyoulizwa  kuhusiana na namna wanaweza kuboresha uandaaji wa filamu ambapo wanafunzi watatu tofauti walijibu kwa ufasaha.
Naye Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bi.Joyce Fissoo alipongeza uongozi wa chuo hicho na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na taasisi hiyo kwa lengo kwa kuwashauri waandaaji wa filamu nchini maarufu kama bongo movie kwenda kusoma katika chuo hicho lengo la kujiongezea weledi katika kazi yao.
‘’Kuna changamoto kubwa kwa waandaaji wa filamu nchini na tumekuwa tukiwaeleza hilo mara kwa mara lakini shida kubwa ni kwa baadhi yao kukosa wa elimu ya kutosha hivyo tutaendelea kutoa msisitizo wa waandaji hao kuhakikisha wafanya kozi mbalimbali za uandaaji wa filamu kwa lengo la kujijengea weledi katika kazi yao’’Fissoo.
Pamoja na hayo Mkuu wa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam Prof.Preksedis Ndomba alieleza kuwa kozi hiyo ya Multi Media kwa mwaka juzi ilikuwa na wahitimu kumi na mbili wa Stashahada na kumi kati yao tayari wameshapata ajira katika sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kwenye vyombo vya habari na kwa mwakani kuna mpango wa kuanzisha shahada.
‘’Darasa hili la Multi Media  limekuwa na changamoto ya rasilimali mbalimbali kama vifaa vya kurekodia wakati wa vipindi sababu darasa hili ni huitwa (smart class) hivyo uendeshaji wa vipindi vyake hutegemea zaidi mtandao,’’Prof.Ndomba.
Halikadhalika Mmoja wa wanafuzi wa Chuo hicho anayesomea Stashahada ya Multi Media Agatha John alieleza kuwa kuputia chuo hicho amepata uelewa mkubwa wanamna ya kuandaa filamu na vipindi kwa vyombo vya habari hivyo anaamini anaweza kufanya kazi hiyo kwa kujiamini na weledi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akipongeza uongozi wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam kwa kuaandaa vijana wenye weledi katika uandaaji wa filamu alipotembelea chuo hicho  jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukutana na wanafunzi wanaosoma kozi ya Multi Media,kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo (kushoto).
 Mkuu wa Chuo cha DIT, Prof.Preksedis Ndomba (kulia) akitoa taarifa ya maendeleo ya kozi ya Multi Media inayotolewa na chuo hicho inavyoweza kusaidia sekta ya filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) alipotembelea chuo hicho jana jinini Dar es Salaam kujionea namna kozi ya Multi Media inaweza kusaidia sekta ya filamu katika uandaaji.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Bibi Joyce Fissoo akiuliza swali kwa baadhi ya wanafunzi wanasoma kozi ya Multi Media katika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (hawapo pichani) namna gani wanaweza kuboresha uandaaji wa filamu, katika ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) chuoni hapo jana jijini Dar es Salaam (watatu kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea chuo hicho kwa ajili ya kufahamu kozi ya Multi Media inavyoweza kusaidia sekta ya Filamu nchini, na wapili kulia ni Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba pamoja na  Katibu Mtendaji  Bodi ya Filamu nchini Bibi Joyce Fissoo (wapili kushoto). Na Anitha Jonas –WHUSM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad