Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 ambayo ni ya 16 tangu kuanzishwa kwake, imezinduliwa rasmi Kibo Palace Homes kwa kushirikisha wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA) na waandaaji wa mbio hizo.
Akizindua mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri kwani wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu kabisa tangu kuanishwa kwake miaka 16 iliyopita na hivi kufanya Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla ifahamike na watu kutaka kupatembelea.
Mkuu wa Mkoa huyo alitoa wito kwa wafanya biashara kutumia fursa hii vizurikwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti kutokana na wingi wa watu huku pia akiwataka washiriki hasa wanaotokea Kilimanjaro kuonesha mfanomzurikwa kushinda zawadi nyingi iwezekanavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira akizindua Kili Marathon 2018 Kibo Palace Homes Moshi huku akiwa na viongozi na wadhamini wa mbio hizo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo ,wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo kampuni ya Tigo inathamini mbio za kilometa 21 almaarufu Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Mbio hizo ambazo hufanyika kila mwaka mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro zitafanyika tarehe 4 Machi mwaka huu.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2018 ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira (Mwenye kofia katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji pamoja na wadhamini wa mbio hizo. Kampuni ya Tigo Tanzania inadhamini mbio za Km 21 almaarufu Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo.

No comments:
Post a Comment