HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 5 January 2018

IGP SIRRO AKAGUA MIRADI KINONDONI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa  Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya  Jeshi hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi.
 Wananchi wa Kigogo Mburahati jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, wakati alipofanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Jeshi hilo Mbweni jijini Dar es salaam katika wilaya ya kipolisi ya Kawe. Picha na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad