HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 3 December 2017

WAZIRI MWAKYEMBE KUHUDHURIA UZINDUZI WA BARAZANI ENTERTAINENT

Na Agness Francis Blog ya jamii
Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe, amehudhuria uzinduzi  wa mradi wa  Barazani Entertaiment  ambapo mradi huo ulianza kutengenezwa miaka minne iliyopita mpaka kufikia hapa ulipo.
Uzinduzi huo umefanyika jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam. Waziri Mwakyembe amewapongeza vijana hao wa bongo muvi walioungana kukamilisha zoezi la mradi huo  ambao unajishughulisha na usambazaji wa filamu ikiwa lengo ni kutaka kukomesha unyonyaji wa wasanii wa bongo muvi hapa nchini.
Aidha Waziri huyo ameongelea changamoto zinazowakabili wasanii hao ni kukandamizwa kimaslai  kutokana  na miundo mbinu za usambazaji wa kazi zao,na kuwata wasanii wote kuunga mkono mradi huu ambao utakuwa ni mkombozi  kwao.
Hata hivyo Meneja masoko na uzalishaji Barazani Entertaiment  Jacob Stiven  amesema kuwa wamejipanga vema katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hizo kwa kila msanii wa filamu anapata haki yake kupitia mradi huo
Nae Msanii wa filamu Jacklen Wolper amewataka wasanii wenzake kuunga mkono mradi huu ili uwe endelevu na pamoja  kuwa na imani na mikakati iliyowekwa ili kuleta mafanikio na mapinduzi ya filamu hapa nchini 
Makamu mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania Jimy Mafufu amemalizia kwa kutoa shukrani kwa ujio wa Barazani Entertaiment na kuitaka pia serikali ya awamu ya 5 kuinga mkono tasnia hiyo na kuiwekea ulinzi ili kukomesha unyonywaji na ukandamizwaji   katika mauzo ya filamu
 Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe akizungumza na waandishi wa wageni waalikwa  kuhusu kazi nzuri inayofanywa  Barazani Entertaiment na kuwapongeza wasanii  hao walioanzisha mradi huo ili kukomesha uuzwaji wa kazi feki za filamu jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa habari utamaduni na michezo Harson Mwakyembe akikata utepe akionyesha kuwa ni ishara ya kufungua rasmi mradi huo jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Afisa utumishi rasilimali watu Barazani Entertaiment Silvana Joseph akitoa risala fupi kuhusu mradi huo  unaohusisha  wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchini ikiwa lengo ni kutokomeza ukandamizwaji wa kazi zao, jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Wageni waalikwa  waliojitokeza katika hudhuria uzinduzi huo kutoka sehemumu mbalimbali jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa filamu Jacklen Wolper akizungumza na waandishi wa habari huku akiwataka wasanii wenzake kuwa na imani katika mradi huo jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.
Meneja masoko na uzalishaji Barazani Entertaiment  Jacob Stiven  akizungumza na waandishi  wa habari juu wa muamko wa wa wasanii katika kuleta maendeleo na kuwataka wale wenye viwanda feki majumbani vya kutengeneza dvd waende kukunua bidhaa kwao ili kuleta usawa katika kipato jana katika ofisi za Barazani Entertaiment Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad