HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 27 December 2017

WAZAZI PELEKENI WATOTO SHULE-NAIBU WAZIRI ULEGA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amesema kuwa changamoto ya wataalam katika halmashauri ya Mkuranga itamalizwa pale wanamkuranga wakiamua kusomesha watoto ambao  ndio watakuwa watumishi wa halmashauri hiyo.
Ulega ameyasema hayo wakati akizindua madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza, amesema uwepo wa changamoto ya walimu na wataalam wengine ni kutokana wanamkuranga kushindwa kutoa kipaumbele katika kusomesha watoto.
Amesema kuwa shule ya awali hiyo ni kwa ajili ya kumuandaa mtoto ili aweze kupata muongozo pale anapoanza darasa la kwanza .
Ulega amesema wananchi wa Mkuranga kwa sasa wanahitaji kuamka katika kusomesha watoto kutokana hali ya uchumi wa viwanda inahitaji wa kada mbalimbali ndio watakaotumikia  uchumi huo bila kufanya hivyo basi wakaotumika katika viwanda hivyo ni kutoka sehemu nyingine kutokana na kuwa na sifa ya kufanya katika viwanda.
Amesema shule zipo cha kufanya wananchi ni kuhimiza kusoma watoto na serikali imeweka mkazo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure ili kila mtu aweze kusoma bila kuwepo kwa kisingizio cha uwezo wa kifedha.
Aidha amesema kutokana ufadhili wa shule ya awali magoza na sehemu nyingine ambayo mfadhili atapita asiwekewe vikwanzo.
Nae Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mkuranga, Ally Msikamo amesema kuwa kazi ya chama ni kusimamia ilani iweze kutekelezeka kama walivyoahidi katika kampeni 2015.
 Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magoza katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya awali katika shule ya msingi Magoza.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza mipango ya halmashauri juu ya uboreshaji wa elimu katika Wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akizindua vyumba vya madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza.
 Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Magoza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega.
Mwonekano wa Madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad