HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 December 2017

WATANZANIA WANAOISHI SAUDI ARABIA WAKUTANA KWA MAJADILIANO

Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia ' Tanzania Welfare Society' hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza. Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mhe. Pandu Amir Kificho alikuwa nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya 'Umrah' katika miji ya Makkah na Madina.

Wanajumuiya walipata fursa ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na Balozi na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi. Vile vile waliweza kuuliza maswali na pia kutoa maoni na ushauri. 

Katika hotuba zilizotolewa wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania. Habari zimeletwa na Mwandishi Maalumu wa Jeddah, Saudi Arabia. Kwa Picha na matukio mengine zaidi angalia youtube kupitia 'Prince eddycool' 
Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanziabar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni mwalikwa, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio mji wa Jeddah Bw. Salim Ali Shatri.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wa Jeddah wakiwa katika picha na meza kuu baada ya mkutano.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad