HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 December 2017

WADAU WALAMBA NONDOZZZ JIJINI DAR LEO

WANAFUNZI 28 wamehitimu shahada za uzamili Utawala wa Biashara na Biashara Kimataifa katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma , Utafiti na Ushauri, Dk. Imanuel Mzava amesema shahada ya uzamili wa Utawala wa Biashara na Biashara Kimataifa inatolewa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Biashara ya Kimataifa ya nchini India (Indian Institute of Foreign Trade)

Amesema kuwa shahada hiyo ilinza kutolewa mwaka 2000 na hadi kufikia leo, wanafunzi 600 wamehitimu katika kozi hiyo na wameendelea kupokea wanafunzi wengine wengi.

Mzava amesema kuwa kuanzishwa kwa shahada hiyo nchini kwa ushirikiano wa Taasisi ya India kumewapunguzia gharama wahitaji wa shahada hiyo ambapo walitakiwa wakasome nchini India lakini elimu hiyo hapa hapa nchini kupitia Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Pichani juu ni baadhi ya wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kulamba nondozz zao, leo katika chuo cha IFM jijini Dar es salaam.
 Mdau Alimwene ambaye pia ni mfanyabiashara akiwa na wahitimu wenzake kabla ya kulamba nondozz hizo.
 Mdau Alimwenye akipamba Nondozz yako na hapa akikabidhiwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma , Utafiti na Ushauri, Dk. Imanuel Mzava. 
 Dada Levina Kato wa Mamlaka ya Bandari pia alikuwa ni mmoja wa waliolamba nondozz.
 Mary Massawe pia kutoka Bandari
 Mdau Morgard Lumbanga 
Mdau Shaban Omary akipokea Nondozz yake kutoka kwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma , Utafiti na Ushauri, Dk. Imanuel Mzava. 
 Wahitimu wakiwa Ukumbini.
 Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Dkt. Satinder Bhatis akizungumza wakati akitoa neno la ufunguzi wa mahafali hayo.
 Baadhi ya wakufunzi wa Chuo hizo wakifatilia mahafali hayo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad