HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 30 December 2017

ULEGA AHIMIZA UJENZI WA SHULE KWA WANANCHI KIJITOLEA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka maafisa maendeleo kutembelea vijijini ili kuhamasisha maendeleo katika kaya za vijiji kutokana na baadhi vijiji kuwa nyuma kimaendeleo. Maana kutofika kwa watendaji kuhamasisha maendeleo kunasababisha wananchi kuona serikali haifanyi kazi.

Amesema kuwa vijiji vikiwezeshwa vitaleta maendeleo kwa haraka kwani serikali ya awamu ya tano inaitaji kusonga mbele bila kumwacha mwananchi yeyote nyuma katika ukuaji wa uchumi.

Akizungumza katika kijiji cha Nyangunguti na Mkenge Kata ya Beta wilayani ya Mkurunga, amesema maofisa wa maendeleo wanatakiwa kukimbizana na kasi ya maendeleo kwani muda wa kukaa ofisini umekwisha.

Amesema ili kuimalisha serikali na kumsaidia Rais Dk.John Pombe Magufuli, watendaji wawe chachu ya maendelwo kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja.

Kwa upade wao wananchi wa kijiji cha Nyangunguti wamemuomba Naibu Waziri huyo kuendelea kuhamasisha maendelea ili vijiji vikue kwa kasi

 Katika ziara ya Vijiji hivyo ameahidi kutoa Mifuko 130 ya saruji, Mifuko 100  kwa ajili ya kuasaidia katika ujenzi wa shule mpya na 30 katika kijiji cha Mkenge kwa ajili sakafu  ya shule ya kijiji hicho.

Aidha ametoa fedha tasilimu sh.100,000 kwa ajili wanafunzi yatima wa kijiji cha Nyangunguti.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Nyangunguti alipowatembelea ili kuhamasisha maendeleo katika kaya za vijiji kutokana na baadhi vijiji kuwa nyuma kimaendeleo
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisalimina na mmoja wa watoa huduka mara baada ya kuwasili katika Zahaniti ya kijiji cha Mkenge Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akionyesha karatasi namna ya udanganyifu wa Korosho unaosababisha soko la zao hilo kuwa na tatizo.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Ulega alipofanya ziara ya kuhamasisha maendeleo katika kaya za vijiji kutokana na baadhi vijiji kuwa nyuma kimaendeleo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad