HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 5 December 2017

Tigo na WorldRemit washuhudia ukuaji mkubwa katika huduma ya kuhamisha fedha katika akaunti za simu za mkononi Tanzania

Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed.
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Hussein Sayed akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kulia ni  Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart.
Meneja Uhusiano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni ya Tigo na ile ya World Remit unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda Tigo Pesa. Kulia ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed na Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit .

WorldRemit na Kampuni ya kidigitali Tigo Tanzania wameshuhudia ukuaji wa kasi wa huduma za kuhamisha fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mkononi nchini Tanzania, taarifa zimebainisha.

Katika kipindi cha miaka miwili cha ushirikiano baina ya kampuni hizi, huduma ya Tigo imebainika kuwa ndiyo huduma ya kutuma fedha inayokuwa kwa kasi zaidi miongoni mwa washirika wa WorldRemit.

Huduma hii inawawezesha Watanzania katika zaidi ya nchi 50 kutuma fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mikononi kwa haraka. Wamiliki wa akaunti za fedha za simu za mkononi pia wanakuwa na uwezo wa kutuma fedha ndani ya nchi, kununua muda wa maongezi, kulipia ankara au kutoa fedha taslimu kupitia mtandao mkubwa wa mawakala wa Tigo.

Licha ya Tanzania kutajwa kuwa ni moja ya nchi ambayo ina gharama kubwa sana kutuma fedha miongoni mwa nchi za Afrika, huduma hii maarufu inapunguza gharama za utumaji wa fedha wakati huohuo ikifanya mchakato wa kutuma fedha kuwa wa haraka na salama zaidi. Upokeaji wa fedha unachukua nafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania. Mwaka 2015 nchi ilipokea zaidi ya dola milioni 400 fedha kutoka nje ya nchi, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

WorldRemit ni mfumo wa kidigitali wa kwanza unaotumia simu za mikononi kutuma fedha unaowaruhusu wahamiaji wanaofanya kazi nje ya nchi kutuma fedha kwa kufuata hatua chache moja kwa moja katika simu zao za mkononi bila kutembelea au kusimama katika foleni kwa mawakala. Kampuni inawajibika kwa 74% ya fedha zote zinazotumwa kupitia mfumo wa kutuma fedha kimataifa kwenda katika huduma za fedha za simu za mikononi.

Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika kutoka WorldRemit, alitoa maoni yake na kusema: “Ushirikiano wetu na Tigo unatoa nafasi zaidi kwa mamlilioni ya watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi kuwa na mbinu mbadala ambayo ni rahisi na salama ya kuwasaidia marafiki na familia zao pasipo kupanga foleni kwa mawakala wa kutuma fedha.”

“Mtanzania aliyehamia London, Stockholm au Sydney sasa anaweza kutuma fedha kuja nyumbani kwa haraka na kwa urahisi – ikiwa inasaidia kuhamisha fedha kwa haraka, usalama na uhakika zaidi kushinda mifumo ya kutuma fedha isiotumia mtandao wa simu inayotegemea mawakala wa kutuma fedha.”

Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa Kampuni ya Tigo Tanzania, aliongezea: “Tigo tumejizatiti katika kutoa huduma kamili ya kifedha kwa wateja wetu. Kama sehemu ya malengo yetu ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kifedha, tunatazamia kuhudumia sio tu soko la ndani ya mipaka ya Tanzania bali pia kwa watanzania wote walioko nje ya nchi. Pamoja na hayo tunachukua hatua zote kuwapatia wateja wetu mfumo wa uhakika na salama kwa ajili ya kutuma fedha kimataifa.”

Kwa sasa wateja wa WorldRemit duniani kote wanafanya miamala 750,000 ya kuhamisha fedha kila mwezi kutoka katika zaidi ya nchi 50 kwenda kwa zaidi ya nchi wapokeaji 148. Tembelea tovuti ya WorldRemit kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kutuma fedha Tanzania.

KUHUSU TIGO TANZANIA

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayoongoza kwa maisha ya Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995 Kupitia bidhaa zake mbalimbali za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, internet yenye kasi na huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi ,Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa Kiswahili, huduma ya TigoPesa, huduma ya simu ya Tigo pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya mipaka ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

Kwa miaka mitatu mfululizo, Tigo ndio kampuni unayokuwa kwa kasi zaidi nchini, na ni kampuni ya pili kwa ukubwa ya uendeshaji wa mitandao ya simu Tanzania. Kupitia mpango wake mkubwa wa upanuaji wa huduma zake, Tigo imezindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es salaam na miji mingine 22 nchini kote kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2016.

Tigo inajivunia watumiaji zaidi ya milioni 11 waliosajiliwa, na imeajiri watanzania moja kwa moja na ambao sio wa moja kwa moja wapatao 350,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wawawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.

Tigo ni Nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara Afrika na Amerika ya Kusini na Ofisi kuu za kampuni zikiwa Ulaya na Marekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad