HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 12, 2017

TARIME NA BUNDA WASHUKURU MFUKO WA HDIF KWA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO KUPITIA UFADHILI WAO


  Kiongozi msaidizi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF), Joseph Manirakiza akimkabidhi barua ya makabidhiano ya mradi na vifaa mganga mkuu wa hospital ya Shirati, Dr. Bwire Chiragi kwa muda wa miaka miwili hospitali hiyo imepata ufadhili wa kuendesha mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto (saving mothers project) katika wilaya za Bunda na Tarime mkoani Mara.
 Mganga mkuu wa hospitali ya Shirati,  Dr. Bwire Chiragi akisaini makabidhiano ya mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto (saving mothers project) katika wilaya za Bunda na Tarime mkoani Mara. Katikati ni kiongozi msaidizi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF), Bw Joseph Manirakiza na Kulia ni Katibu wa hospitali ya Shirati, Ogottu Obala.
 Msaidizi kiongozi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF) , Joseph Manirakiza (katikati) akifafanuliwa jambo na viongozi wa hospitali ya Shirati iliyopo mkoani Mara, kulia ni Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Dr. Bwire Chiragi na kushoto Katibu wa hospitali hiyo, Juma Ogottu Obala

 Baadhi ya Baiskeli 124  zilizotolewa na Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF) uliochini ya UKAIDS kwa ajili ya kuwasaidia wauguzi katika Wilaya ya Bunda na Tarime.
 Mama Prisca  Koboko  Ambae ni muuguzi toka Tarime akielezea jinsi mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto ulivyowawezesha kuwafikia wakina mama.
Mama Teodocia  James, wa kwanza kushoto ni mmoja ya wamama walionufaika na huduma za mradi huu wa 'Saving Mothers' uliopata ufadhili wa HDIF kwa karibu shilingi bilioni moja   ya Tanzania akielezea jinsi mradi ulivyookoa maisha yake.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF)  kwa hospitali ya Shirati kuhakikisha juhudi za kuokoa maisha ya mama na mtoto zinaendelezwa hata baada ya mradi kuisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad