HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 December 2017

TAKUKURU yamfikisha mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis.
Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amefikishwa leo Jumatatu Desemba 11,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa makosa mawili.
Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga alisema jana Jumapili Desemba 10,2017 kuwa Sadifa angefikishwa mahakamani leo.
Alisema kiongozi huyo alikamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kwa kuwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka Mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume cha maadili.
Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa Sadifa alisema alikamatwa Jumamosi Desemba 9, 2017.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad