Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baraza la Ushauri la walaji la Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA –CC) imesema kuwa hakuna kupandisha nauli na watakaopandisha nauli watakuwa wamekiuka masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa SUMATRA-CC , Dk. Oscar Kikoyo amesema kuwa kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kuna baadhi wamekuwa wanakiuka leseni zao.
Amesema kuwa wananchi wanaosafiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa baadhi ya basi ambazo zinapandisha nauli ili hatua zichukuliwe katika kukomesha suala hilo.
Dk. Kikoyo amesema kuwa na wale ambao wanachukua tiketi za basi na baadaye kuuza kwa abiria kwa bei ya juu, abiria wanatakiwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili kuchukuliwa hatua kwa mmiliki wa basi.
Aidha amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano pale wanapoona watu wanauliza ndani ya basi juu masuala mbalimbali ili kubaini vitu ambavyo vimekwenda nje ya utaratibu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la walaji la Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA –CC) , Dk. Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi habari kuhusu masuala mbalimbali ya usafirishaji wa abiria kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment