HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 13, 2017

RAIS WA PALESTINA AMSHUKURU PAPA FRANCIS

 Rais wa Palestina Mheshimiwa “Mahmuud Abbas” katika hotuba yake kwenye Mkutano wa dharura wa Kiislamu uliofanyika nchini Uturuki, kujadili azimio la Rais wa Marekani Donald Trump la kuitambua Jerusalem kuwa ni mji mkuu wa Israeli, amemshukuru Papa Francis, nchi zote na viongozi wa nchi hizo, waliotangaza kwa pamoja msimamo wao wa waziwazi na unaopinga matendo yasiyofaa ya Rais wa Marekani, huku wakisimama kidete na wananchi wao dhidi ya azimio hilo lisilo la kisheria.
Aidha, Rais Abbas ameweka wazi ya kwamba taifa la Palestina na mataifa yote kiarabu, wakiwemo waislamu na wakristo wanaungana katika kulikabili azimio hili lisilo sahihi na linalokwenda kinyume na maazimio yote ya Baraza la Usalama, Mahakama ya Kimataifa ya Haki na maazimio ya Mashirika yote ya kikanda na kimataifa, yanayoshughulikia mgogoro wa Palestina na Israeli yakiwemo maazimio ya Umoja wa Afrika.
Rais Mahmuud Abbas  wa Palestina  pia ametilia mkazo kuwa, hakuna amani itakayopatikana bila ya kutambulika Jerusalem ya mashariki kama ni mji mkuu wa dola ya Palestina na kwamba Wananchi wa Palestina wataendelea kusimama kidete katika ardhi yao na kulinda sehemu takatifu za kikristo na kiislamu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad