Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakishiriki kufanya usafi katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa, Joel Festo akikabidhi zawadi ya Vyandarua kwa Mratibu wa kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai akikabidhi zawadi ya Vyandarua kwa Mratibu wa kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Amani Street Children Centre kilichopo katika Manispaa ya Singida.
Na Anthony Ishengoma
Wajumbe wa Balaza la Watoto la Taifa leo wameungana na watoto wanaotunzwa katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani Amani kilichopo katika Manispaa ya Singida ili kuwafariji na kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kuishi katika familia kama ilivyo kwa watoto wengine wanaoishi na wazazi wao.
Watoto hao wanalelewa katika kituo hicho baada yakuwa wamejiingiza mjini na kuanza maisha kabla ya wakati jambo ambalo uwalazimisha kuishi katika mazingira hatarishi ikiwemo wizi na kuvutishwa bangi na madawa ya kulevya.
Mkuu wa kituo cha kulelea watoto hao katika kituo cha Amani Street Children centre Bi. Getruda Kifumu ametaja chanzo cha kuongezeka kwa watoto wa mitaani kuwa ni umasikini wa kipato katika familia, ugonvi katika ndoa, kuachana kwa familia ikiwemo imani potofu ya kuwa mjini kuna nafuu ya maisha.
Aidha Bi. Getruda amesema kituo chake kina zaidi ya watoto 50 ambao tayari wamerudishwa kwa familia baada ya kuwa wamezungumza na familia lakini pia na watoto wenyewe japokuwa baadhi ya watoto utoroka.
Amesema kituo kinakaa na watoto kwa miezi tisa na baada ya hapo uwarudisha kwa familia zao na kuendelea na maisha na kukukiri kuwa baadhi ya watoto uweza kurejea mitaani na kulazimika kurudishwa kituoni hapo.
Bi Getruda ameongeza kuwa changomoto iliyopo ni kuwa watoto wengine wanakuwa na umri mkubwa hivyo kupata changomoto ya kuwarudisha katika mfumo rasmi wa shule na sababu inayowafanya baadhi yao wasiendelee kimasomo.
Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Nchini Bi. Margaret Mussai ameviambia vyombo vya kuwa utafiti wa shirika la kimataifa la watoto UNCEF wa mwaka 2016 unasema Tanzania ina watoto elfu35 wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Amezija sababu za kuwepo hali hiyo hapa Nchini kuwa ni watoto kukosa malezi bora toka kwa familia zao kwa kuwa utafiti pia unaonesha asilimia 60 ya vitendo vya ukatiri vinatokana na familia za Watoto akitaja vitendo vya kulawiti watoto vimeripotiwa kuhusisha ndugu wa karibu na watoto.
Amezitaja sababu nyingine kuwa umasikini na wazazi kuangaika zaidi kutafuta fedha na kusahau majukumu ya kulea watoto wao jambo linalopelekea watoto kuiga kila jambo kutoka mitaani badala ya kupewa miongozo ya maisha na wazazi wao.
Mkutano wa Baraza la Watoto Taifa unaendelea leo mjini Singida agenda kubwa ikiwa ni kufanya uchaguzi wa wawakilishi wawili watakao liwakilisha Taifa katika mkutano wa kimataifa wa watoto utakaofanyika mapema mwakani Nchni Sweden.
No comments:
Post a Comment