HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 24 November 2017

WAZIRI KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI LEO

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Jasem Al Najem tarehe 24 Novemba, 2017.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza masula mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri Kairuki amesema kuwa mazungumzo yake na Balozi wa Kuwait yamelenga katika suala la uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ambapo ameikaribisha nchi hiyo kuja kuwekeza nchini ili kuendeleza Sekta husika.
Aidha, ameongeza kuwa, katika kikao hicho wamezungumzia suala la kuwajengea uwezo Wataalam wa Madini nchini ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Vilevile wamejadiliana suala la kubadilisha uzoefu kati ya Kuwait na Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika uchumi wa nchi husika.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akiwa na Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kushoto),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akipokea zawadi ya Ngao kutoka kwa Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia),  katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al-Najem (kulia) akimweleza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) kuhusu alama mbalimbali zilizo katika Ngao kutoka nchini Kuwait, mara alipomtembelea katika ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad