HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 18 November 2017

WANANCHI WAANDAMANA HARARE KUSHINIKIZA RAIS MUGABE AJIUZULU

Wananchi wa Zimbabwe waliojawa na furaha wameandamana katika Jiji la Harare wakishinikiza rais Robert Mugabe ajiuzulu.

Waandamanaji hao wameonekana wakiwakumbatia wanajeshi kuwapongeza kwa uamuzi wa kuchukuwa udhibiti wa nchi hiyo tangu jumatano.

Maandamano hayo yanaungwa mkono na wanajeshi na wanachama wa chama tawala wa Zanu-PF, huku maveterani wa vita nao wakimtaka Mugabe aachie madaraka.
Wananchi wa Zimbabwe bila kujali rangi zoa ama itikadi za vyama vyao wakiandamana mitaani
Waandamanaji wakiwa na picha za Mkuu wa Majeshi Jenerali Constatino Chiwenga pamoja na Makamu wa Rais Emerson Mnangagwa katika kuwapongeza 

Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad