HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 22 November 2017

WADAIWA SUGU WA KAMPUNI YA TTCL WAPELEKWE MAHAKAMANI- NAIBU WAZIRI MHANDISI NDITIYE

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea makao makuu ikiwa ni mara ya kwanza na kuwataka kuwachukulia hatua wale wote wanaodaiwa madeni sugu. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Mary Sassabi. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 
NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara makao makuu ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) na kuwataka kuwachukulia hatua wadaiwa sugu ikibidi kuwapelekea mahakamani kwa mujibu wa sheria. 

Akizungumza mbele ya menejinenti ya TTCL, Mhandisi Nditiye amesema kuwa wale wanaodaiwa na hawafuati taratibu za kulipa madeni wanatakiwa wapelekwe mahakamani na zaidi wadaiwa hao bado wanaendelea kutumia huduma za TTCL. 

Mbali na hilo, Mhandisi Nditiye amesifia huduma ya Conference Video Call kwani itasaidia kupunguza gharama kwa serikali na itaruhusu watu kufanya mikutano kupitia njia ya mawasiliano na sio kukutana kama ilivyokuwa zamani. 

"Huduma hii ya Conference Video Call itasaidia kupunguza gharama kwa serikali ambapo awali ilikuwa unatakiwa kuwakusanya viongozi wote 

Kuja katika mkutano ila kwa huduma hii unaweza kuzungumza nao wakiwa huko huko waliko," amesema Mhandisi Nditiye. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba akielezea namna kampuni yao ilivyowez akukusanya deni la bilioni 6.8 kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kwa wadaiwa sugu huku akimuelezea Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye namna Conference Video Call inavyoiweza kufanya kazi. 

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba amesema kuwa kwa sasa TTCL inatekeleza mpango mkakati wa mageuzi ya kibishara na ni mahsusi kwa mabadiliko ya kuwa kiongozi wa huduma za mawasiliano na TEHAMA katika soko la Tanzania. 

Kindamba amesema wanamatumaini kuwa mchakato wa kupata sheria mpya ya kampuni ya TTCL kuja kuwa Shirika la Mawasiliano iliyopitishwa na bungeni wiki iliyopita unaweza kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli. 

Kampuni ya TTCL imeweza kukusanya takribani bilioni 6.8 za madeni ndani ya miezi mitatu ambapo awali deni lilikuwa ni Bilioni 10.7. 

Kwa sasa, TTCL imeweza kuboresha huduma zake kwa takribani mikoa 18 ikiwemo Unguja na Pemba pamoja na kutumia teknolojia za kisasa za 2G, 3G, 4G na FMC pia kuwa na huduma za TTCL PESA.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa anaongea na wafanyakazi wa kampuni ya simu (TTCL) kutoka Dodoma kwa njia ya Conference Video Call. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad