HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 November 2017

VIONGOZI WA MRADI WA UTAFITI WA AFYA YA MALIASILI MAJINI, TRAHESA, WAKUTANA NA MAKAMU WA MKUU WA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO(SUA).

Makamu wa Mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, Prof Raphael Chibunda amewahakikishia viongozi wa mradi wa utafiti unaoshughulika na afya ya maliasili za majini, TRAHESA, kupewa kila aina ya msaada na SUA ili kufanikisha malengo yake kwa manufaa ya nchi husika na ulimwengu kwa jumla.
Hakikisho hilo limetolewa leo kufuatia viongozi wa mradi wa TRAHESA kumtembelea Makamu wa mkuu wa Chuo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada ya uteuzi wa Prof. Chibunda mapema mwaka huu.
Amesema mradi huo wa utafiti wa afya ya maliasili za majini wakiwemo samaki utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi washiriki pamoja na dunia kwa ujumla kwa vile hakujakuwepo kwa tafiti za kutosha za maliasili za majini katika nchi za mashariki na kusini mwa Afrika.
Kiongozi Mtafiti wa mradi wa TRAHESA Prof. Robins Mdegela akiongozana na maafisa kutoka nchi mfadhili Norway na nchi washiriki katika mradi za Kenya, Uganda, Zambia na mwenyeji Tanzania wapo katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, kwa kikao cha kawaida cha mradi kufuatia SUA kuchaguliwa kama nchi mwenyeji wa mradi tangu ulipoanzishwa mwaka 2014.
Prof. Mdegela amesema katika mradi huo wa utafiti wanajumuisha pia wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu kutoka nchi zinazoshiriki katika mradi na wanadhaminiwa kufanya tafiti mbalimbali kuhusiana na afya za maliasili za majini wakiwemo samaki na mimea majini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad