HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 8, 2017

UZINDUZI WA ZOEZI LA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA WAFANYIKA MKOANI MTWARA


 Katibu tawala wa mkoa wa Mtwara akisisitiza jambo kwa wenye wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara na baadhi ya wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara ambalo linatarajiwa kuanza rasmi mwanzoni mwa wiki ijayo 
 Kaimu mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi. Rose Joseph akiwasilisha salamu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndg, Andrew Wilson Massawe kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara  pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, watumishi wa NIDA pamoja na wageni wengine waalikwa. 
 Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa pichani wakisikiliza jambo kutoka kwa mwakilishi Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa sherehe ya uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Mtwara pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara
 Afisa usajili msaidizi wa NIDA Ndg. Fredy Mahundi akifanya zoezi la usajili kwa mara ya kwanza kwa mwananchi wa mkoa wa Mtwara mara baada ya zoezi la uzinduzi wa usajili kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kukamilika.
Bi Amina Bakari akichukuliwa alama zake za Vidole ambapo alipata nafasi ya kuwa mwananchi wa kwanza kusajiliwa kwa mkoa wa Mtwara mara baada ya zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa Mtwara kukamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo amezindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa wananchi wa mkoa huo tayari kuanza rasmi kwa zoezi la usajili kwa wananchi ikihusisha kuchukuliwa picha, saini na alama za Kibaiolojia.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Mtwara umejipanga na uko tayari kwa zoezi hilo, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa hali na mali kuhakikisha hakuna mwananchi yeyote mwenye sifa ambaye ataachwa bila kusajiliwa.
Katika sherehe za uzinduzi rasmi wa zoezi hilo zilizofanyika makao makuu ya Mkoa  huo Mtwara; zilihudhuriwa na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Meya, Katibu Tawala Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mkoa, Watumishi katika ngazi mbalimbali na vyombo vya Habari.
Akizungumza kwa niaba ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Joseph ameeleza Mamlaka imejipanga kuanza rasmi zoezi hilo Jumatatu tarehe 13 Novemba, 2017 na wanakusudia kukamilisha zoezi hilo kwa mkoa wa Mtwara kufikia Februari 2018 na kuanza kutoa namba za Utambulisho NIN sambamba na uzalishaji wa Vitambulisho.
Ziadi ya wananchi mil 1,250,000 wanatazamiwa kusajiliwa mkoani humo. Mikoa mingine ambayo usajili umeanza ni Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Arusha, Shinyanga, Geita, Mwanza, Simiyu, Manyara na Songwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad