HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 3 November 2017

TFDA YAPATA CHETI CHA UBORA WA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA 1SO 9001.2015

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imepata cheti cha mfumo wa uhakiki wa Ubora wa Huduma cha Kiwango cha kimataifa cha ISO  9001.2015  na kufanya mamlaka hiyo kuwa ya pili katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema kuwa mafanikio ya TFDA ni kutokana na kazi  wanayofanya katika udhibiti dawa na chakula kwa ajili ya kutumia bidhaa zenye ubora.
Amesema kuwa TFDA ni mamlaka ambayo inagusa masilahi ya kila mtu na hakuna asiyetumia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni kulinda afya za wananchi ambao wanaweza kufanya kazi na kuiletea taifa maendeleo hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Dk. Ndugulile amesema kuwa TFDA kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa chakula, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ni utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali ya awamu ya tano chini uongozi mahiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha upatikanaji wa wa huduma bora za afya hususani  upatikakanaji wa dawa , vifaa tiba na vitandanishi.

Aidha amesema nyenzo zilizofanya mafanikio katika udhibiti ni maamuzi ya menejimenti zaidi ya miaka 10 wa kudhamiria kutekeleza mfumo wa uhakiki ubora wa huduma .
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema kuwa katika kuongeza huduma za udhibiti kwa wananchi wameanzisha ofisi saba za kanda ambazo zitahudumia katika mikoa iliyopo katika kanda hizo.
Sillo amesema kuwa mamlaka imekuwa ikitekeleza mfumo wa uhakiki ubora kuanzia mwaka 2005 baada ya kufanya tathimini ya namna bora ya kufanya shughuli za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo (wakatikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye piha ya pamoja wakati akizindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad