HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 November 2017

STARTIMES YAJA NA MFALME WA FAMILIA

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes ambayo imeidhinishwa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Moja kwa Moja, msimu huu wa Sikukuu imekuja na Ofa ya aina yake kwa wateja wake pamoja na wateja wapya watakaopenda kujiunga na huduma za kampuni hiyo.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja wa Uhusiano na Masoko Bw. Juma Suluhu alisema kuwa kampuni ya StarTimes inatambua umuhimu na uzito wa Kipindi hiki cha Sikukuu kwa watanzania hivyo wao kama Kampuni wamejipanga vyema kutoa burudani ambayo ya kiwango cha hali ya juu.
“Tumewaletea watanzania Ofa tuliyoipatia jina la ‘Mfalme wa Familia’, tumeiita hivyo kwa sababu sisi ni wafalme wa Burudani za Familia, ukianzia filamu, michezo kama mpira wa miguu, kikapu, katuni, Muziki, Ndondi na vingine vingi. Tuna vipindi ambavyo watoa huduma wengi hawana, hivyo ni fursa ya kipekee kwa watanzania kufurahia.”
Ofa hii inaenda sambamba na kushuka bei ya king’amuzi cha Antenna ambacho awali kilikuwa kikiuzwa kwa Tsh 47,000 sasa kitapatikana kwa bei ya punguzo Tsh. 34,000 pekee. “Ofa yetu ina mambo makubwa matatu, Jambo la kwanza ni hilo punguzo la bei ya king’amuzi cha Antenna, pili ni king’amuzi cha Combo ambacho kinatumia dish na Antenna ambacho awali kilikuwa kikiuzwa kwa Tsh 86,000 sasa kitapatikana kwa Tsh 78,000 huku mteja atakayenunua atapata kifurushi cha Mwezi mzima pamoja na Dish Bure”, alisema Juma.
“Tatu ni luninga zetu za kidigitali, hapa unapata vitu vitatu, cha kwanza luninga zetu zina king’amuzi ndani, cha pili ukinunua luninga yetu unapatiwa dish bure na cha mwisho utaunganishwa kifurushi cha Uhuru kwa mwezi mmoja Bure”, aliongeza.
Licha ya Ofa hizo kabambe bado wateja wa StarTimes wataweza kupata Chaneli zote za Kifurushi cha Kili katika kifurushi cha Uhuru kuanzia tarehe 1 Disemba ikiwa ni sehemu ya Promosheni ya Mfalme wa Familia ambayo imeletwa na StarTimes Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad