HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 1, 2017

SPIKA NDUGAI, KATIBU WA BUNGE, NDG. KAGAIGAI WATEMBELEA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII.

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akiwasili na kupokelewa na  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Ndg. Sebastian Kapufi (kulia) kabla ya kuanza kikao na kamati hiyo kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakifuatilia kikao cha pamoja cha kamati hiyo walipotembelewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake. katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma.

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai na kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa, Sebastian Kapufi.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. wa tatu kulia ni Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa, Sebastian Kapufi.

 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia kikao cha kamati hiyo walipotembelewa na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai kwa lengo la kuangalia jinsi kamati hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kilichofanyika leo ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, uliopo Mjini Dodoma. kushoto ni Mheshimiwa Mary Chatanda, katikati ni Mheshimiwa Atupele Mwakibete na kulia ni Mheshimiwa Neema Mgaya.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad