HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 2 November 2017

SIMBA HAOO.....KUELEKEA MBEYA KUZIFUATA POINTI 6


KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya michezo miwili ya  ligi kuu Vodacom dhidi ya Mbeya City na Prison huku  kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog akiweka wazi kuwa anataka kuvunja rekodi ambayo ni kuibuka na pointi sita kwenye michezo miwili mbele ya wapinzani wao, Mbeya City na Prisons.

Omog na jeshi lake la Simba litakuwa na kibarua kigumu cha kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mara kwa mara wamekuwa na matokeo mabaya, ambapo Jumapili watawavaa Mbeya City kwenye uwanja huo kisha kumaliza na Prisons, Novemba 18, mwaka huu.

Mcameroon huyo amesema pamoja na rekodi mbaya kila wanapocheza uwanjani hapo lakini safari hii hawataruhusu hilo litokee kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu za kila mchezo.

“Tunajua kuwa mara kwa mara tunasumbuka kupata matokeo hapa Sokoine, lakini safari hii sitakubali kuona hilo linatokea tayari tumeshaweka mikakati kabambe ya kupata pointi sita kutoka kwa wenyeji wetu".

“Tunataka tushinde kwa ajili ya kujiongezea wigo wa pointi dhidi ya mahasimu wetu ambao tunalingana nao kwenye msimamo, na hatuwezi kuwakimbia bila ya kupata matokeo mazuri hasa kwenye mechi kama hizi za ugenini.

“Niseme wazi kwamba lile suala eti la kuwa na rekodi ya kupoteza mechi kila tunapokuwa hapa Mbeya kwa sasa ndiyo limefika mwisho,” alisema kocha huyo.


Mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally alisema taratibu zote za kukamirisha safari hiyo zimekamilika.“Timu inatarajiwa kuondoka jijini Dar kesho saa tatu kamili asubuhi na ndege tukielekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Mbeya City na Prison.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad