HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 7 November 2017

SAMATTA NJE WIKI SITA, AUMIA GOTI SASA KUWAKOSA BENIN NOV 12


NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anayekipiga na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atakuwa nje ya uwanja kwa majuma sita akiuguza majera ya goti aliyopata katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa sare tasa dhidi ya Lokeren.

Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada kuumia dakika ya 40 nafasi yake ikachukuliwa na Nikos Karelis aliyerejea hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu pia kutokana na majeraha.

Ripoti ya daktari iliyotokana na majibu ya vipimo alivyofanyiwa straika huyo jana inasema amepata jeraha dogo katika misuli ya goti inayofahamika kitaalamu kama ‘Literal Ligament’ huku pia maungio ya mfupa wa paja na wa ugoko (meniscus) yakionekana kuathirika pia.

“Literal ligament imechanika kidogo, hiyo itapona yenyewe lakini pia wamegundua tatizo kwenye meniscus ambalo inabidi lifanyiwe upasuaji mdogo ili lisije kuleta shida hapo baadae,” alisema Samatta

Upasuaji huo mdogo utamlazimisha Samatta kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita akipata tiba na mazoezi huku timu yake ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Ubelgiji baada ya kukusanya pointi 19 pekee.

Samatta ndiye mshambuliaji tegemeo klabuni hapo akiwa amejihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuwepo kwa wakali kadhaa.

By Boiplus Media.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad