HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 2, 2017

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWAPONGEZA TANROADS KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani Kigoma.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (hayupo pichani) katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia), mkoani Kigoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Samson Hanga akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani humo.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakiimba wimbo wa mshikamano katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa katika Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala huo, lililofanyika mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.
Akifungua Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.
“Hakikisheni kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria anachukuliwa ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Naye Mtendaji Mkuu Wa Wakala huo Eng. Patrick Mfugale, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja watumishi 71  wamefukuzwa kazi katika vituo mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Ameongeza kuwa TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo vya mizani vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini kwa wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.
Wajumbe wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote  nchini wamekutana katika mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini utendaji kazi wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad