HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2017

MUFINDI YANUNUA MAGARI KWA MAKUSANYO YA NDANI

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekamilisha mpango wake wa kununua Magari Mawili (2) mapya kwa kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani ya mwaka wa fedha 2016-2017 uliyokamilika mwezi juni mwaka huu.

Taarifa ya kitengo cha habari na Mawasiliano cha Halmashauri hiyo, imeyataja Magari hayo kuwa ni Toyota Landcruiser Standard kwa gharama ya Sh. 187,680,373.11na Toyota Hilux –Double Cabin kwa gharama ya Sh. 93,450,713, ambapo Magari yote mawili yamegharimu Sh. 281,131,086.11.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Magari hayo yamenunuliwa ili kukabiliana na changamo ya uchakavu na upungufu mkubwa wa Magari uliyopo na kutanabaisha kuwa kati ya Magari hayo, gari ya kwanza itatumiwa na Ofisi ya utala ambayo wakati wote hutakiwa kufika kila kona ya eneo pana la Halmashauri lenye Majimbo mawili kata 27, Vijiji 121 na Vitongoji 562 kusimamia shughuli za maendeleo, huku gari ya pili ikinunuliwa mahususi kwa shughuli za kukusanya Mapato.
Aidha, Mchakato wa Manunuzi wa Magari hayo ambayo ni moja kati ya nyenzo muhimu za kuharakisha maendeleo katika Halmashauri ya Mufindi, umefanyika kwa kufuata taratibu zote za manunuzi ya Umma, ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha kufanya manunuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati mchakato mzima wa kuyanunua ukitekelezwa na taasisi za zilizokasimiwa jukumu la manunuzi ya Umma, ambazo ni TEMESA na GPSA.
Afisa manunuzi wa halmashauri Mr. Katunzi akikabidhi funguo za gari pamoja na nyaraka za umiliki kwa Mkurugenzi Mtendaji ambapo naye atakabidhi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri.
 Mkurugenzi Mtendaji Prof. Riziki Shemdoe, kulia katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halamshauri Festo Mgina mara baada ya kupokea nyaraka za umiliki wa Magari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad