HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 9, 2017

MKUU WA MKOA WA GEITA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MGANZA WILAYANI CHATO


Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga ukuta katika kituo cha afya Mganza Halmashauri ya Wilaya Chato.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mganza (Chato) alipofanya ziara ya kikazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.

Akina mama wa kijiji cha Ilyamchele Wilayani Chato wakishiriki katika ujenzi wa vyumba viwili na Ofisi shule ya Msingi Ilyamchele kwa kusogeza matofali kwa mafundi wa ujenzi.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchimba msingi wa kujenga vyumba viwili na ofisi na wananchi wa kijiji cha Ilyamchele (awapo kwenye picha)katika uzinduzi wa kampeni ya kujenga vyumba vya madarasa na zahanati Wilayani Chato.

NA JOEL MADUKA
Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa Zahanati Wilayani Chato ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Wilayani humo.

Mhandisi Robert Gabriel amezidua kampeni hiyo kwa kushirikiana na wananchi kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa viwili pamoja na Ofisi katika shule ya msingi Ilyamchele ambayo inaongezeko la wanafunzi 2,212 kutoka 1,700. Darasa la pili linawanafunzi 407 ambao wanasoma kwa awamu mbili hivyo, kufanya shule hiyo kuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 28.
Akizungumza na wananchi baada ya kuchimba msingi Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Serikali inataka watoto wa Ilyamchele wafanane na watoto wa maeneo mengine kwa kukaa katika vyumba vizuri vya kisasa vyenye miundombinu ya kutosha na walimu wa kutosha. Hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na viongozi wote katika utekelezaji wa miradi hii ili kumaliza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amendelea na ziara hadi kijiji cha Mganza ambapo ameshiriki katika ujenzi wa kituo cha afya Mganza ili kuona hali ya wananchi kupata huduma katika vijiji inaimalika kwa kujenga Zahanati na vituo vipya vya afya.

Miradi hii inatekelezwa na vikundi vya mafundi walioungana kwa kujitolea kufanya kazi hiyo pasipo kuwa na malipo isipokuwa kupatiwa chakula wanapokuwa katika eneo la kazi. Wananchi na wadau wanashiriki kwa kuleta maji, mchanga, sementi, kokoto na kushiriki katika ujenzi. 

Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa baada ya kuwasili mkoani Geita baada ya uteuzi wake aliamua kutoa semina kuhusu mikakati na njia za kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Tarafa, Maafisa elimu wa Wilaya na Makatibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad