HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 November 2017

KWANDIKWA AWATAKA TEMESA KUANZA MARAMOJA MATUMIZI YA MFUMO WA KIELETRONIKI

Abiria wakiingia katika Kivuko cha MV Kazi kinachoendelea kutoa huduma za usafiri kati ya Magogoni na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuanza kufanya majaribio ya uboreshaji wa mashine za mfumo wa kielektroniki za kukatia tiketi ili kurahisisha zoezi hilo na kulinda mapato sahihi ya Serikali.

Akikagua huduma zinazotolewa na vivuko katika maeneo ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Kwandikwa amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ya usafiri kwa viwango vya kisasa na muda mfupi.

“Hakikisheni mfumo huu unaanza kujaribiwa mapema iwezekanavyo ili kama kuna upungufu utakaojitokeza mkandarasi aushughulikie mara moja kabla ya kipindi cha uangalizi hakijamalizika”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Ameongeza kuwa uboreshaji wa mfumo wa kieletroniki wa kukatia tiketi utasaidia kudhibiti ukusanyaji wa mapato na kutunza kumbukumbu sahihi za abiria wanaopata huduma katika maeneo hayo.

Aidha Naibu Waziri Kwandikwa, amewataka TEMESA kuongeza matangazo ya elimu kwa wananchi ya namna ya kuchukua tahadhari wanapotumia vivuko hivyo ili kuongeza uelewa na kuepusha ajali.

Kuhusu huduma zinazotolewa na vivuko vya Mv. Magogoni, Mv. Kazi na Mv. Kigamboni, mtumiaji wa vivuko hivyo Bw. Riziki Phillipo, amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha usafiri kati ya Magogoni na Kigamboni unakuwepo kwa uhakika na wakati wote.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na mmoja wa wafanyakazi mara baada ya kukagua uboreshaji wa mashine za mfumo wa kielektroniki za kukatia tiketi eneo la Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa mambo ya kiufundi kutoka kampuni ya Maxicom Africa Bw. Peter Mungo, wakati akikagua uboreshaji wa mashine za mfumo wa kielektroniki za kukatia tiketi eneo la Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Vivuko Bernad Daud, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, wakati akikagua hali ya uendeshaji wa vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la Magogoni na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na baadhi ya abiria wanaopata huduma za vivuko katika eneo la Magogoni na Kigamboni, wakati alipofanya ziara yake kuona huduma zinavyotolewa na vivuko hivyo, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad