HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 20, 2017

ESRF YATAFUTA SULUHU YA UTENGENEZAJI MIJI

MANUFAA ya uchumi unaokua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda hayataonekana kama taifa litakuwa na changamoto katika utengenezaji wa miji yake na hivyo kuvuna tija ya miji iliyopangwa vyema.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy wakati akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuangalia mada tatu zilizokubaliwa kufanywa kama sehemu ya kutengeneza mwongozo wa namna ya kuendesha mpango huo ili kuisaidia serikali katika kutengeneza miji salama na yenye tija.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mada hizo tatu ni pamoja na kuangalia miundombinu ya miji na huduma za kifedha katika utengenezaji wa miji, mahusiano ya serikali kuu na ya mitaa ; na mada ya tatu ni namna ya kupata taarifa sahihi ili kuimarisha uwekezaji.

Kessy alisema wakati serikali inatekeleza malengo ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDP) ll , wenye lengo la kuweka mazingira sawa kwa uchumi wa viwanda na maendeleo, mpango huo wa ESRF umekuja muda muafaka kwani utasaidia kutafuta na kutoa majawabu halisi na sahihi.
Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy akifungua mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema kwamba kama nchi itataka kuwa na maendeleo yenye kujali binadamu ni vyema kuwa na maamuzi ya miongo yenye kuakisi uhalisia na mahali pekee kwa sasa kupata huo uhalisia ni wa kutumia mpango huo wa ESRF ambapo wanazuoni watakutana kujadili uhalisia wa mambo na kutoa mapendekezo ya kukabili changamoto.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida alisema mkutano huo ambao ni wa kwanza tangu alipoamua kuwa na Tanzania Urbanisation Laboratory, Agosti mwaka huu umelenga kusaidia kutengeneza njia ya kusaidia utengenezaji wa miji salama yenye tija nchini.

Alisema kwa kuwa mwenyekiti wa mpango huo ni Tume ya Mipango wao wakiratibu tu, ni dhahiri mawazo na mapendekezo yatakayokuwa yanatolewa kulingaana na utafiti yatasaidia sana kuwa na miji salama.
Pichani juu na chini ni Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akitoa mada ya utangulizi wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole (kulia) akiwasilisha mada kuhusu kuwelewa upangaji wa miji na namna fedha zinavyopatikana wakati mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dr. Wilfred Lameck, akiwasilisha mada Utafiti kuhusu mahusiano ya serikali kuu na serikali za mitaa Tanzania wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Dr. Nathalie Jean-Baptiste kutoka Taasisi inayoshughulikia makazi ya watu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, akiwasilisha mada kuhusu maisha ya kila siku ya watanzania katika miji wakati wa wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Pichani juu na chini ni washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Paul Kessy akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida.
Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Dr Kate Owens kutoka World Resources Institute ya Marekani akitoa neno wakati wa kufunga mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Pichani juu na chini ni washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) akibadilishana mawazo na Bw. Anton Cartwright (katikati) kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini pamoja Dr. Kate Owens kutoka World Resources Institute wakati wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa wanazuoni walio katika Mpango wa Fikira za Uendelezaji wa Miji Tanzania (Lab Tanzania) unaoratibiwa na taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad