HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 1 November 2017

CRDB YAWAPA AHUENI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU DODOMA

Ikiwa ni msimu mpya wa ufunguzi wa vyuo mbalimbali nchini, Benki ya CRDB imewapa ahueni kubwa wanafunzi wa elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kwa kusogeza huduma za kibenki katika maeneo yanayotumika kufanya usajili wa wanafunzi. Kupitia matawi yake yanayotembea na wakala wa benki (FahariHuduma), Benki ya CRDB imeweza kupeleka huduma za kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.

Ukiondoa huduma za kuweka na kutoa fedha, zoezi la ufunguzi wa akaunti maalum ya wanafunzi ya Scholar limekua likifanyika ili kuwawezesha wanafunzi hususani wale wanaopokea mikopo ya elimu ya juu kuweza kutunza fedha zao kwa usalama. Katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho kina jumla ya vitivo saba ndani yake, Benki ya CRDB imeweza kusogeza huduma za kifedha katika vitivo vyote saba pamoja na kuwa na tawi na mashine za kutolea fedha katika vitivo vyote.

Akizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Dodoma Ikupa Mwambene amesema, “tunaishukuru sana Benki ya CRDB kwa kuweza kutusogezea huduma hadi katika vitivo vyetu kwani imeweza kuturahisishia zoezi kufanya usajili na kuokoa muda mwingi”. Nae Afisa Uhusiano wa chuo hiko Bi. Beatrice Baltazar amesema kuwa uwepo wa huduma za benki zinatozolewa na Benki ya CRDB umeweza kuwapa unafuu mkubwa wanafunzi kwa kuwa ilikua ikiwalazimu kwenda nje ya chuo kufata huduma za kibenki kasha kurudi chuoni ili kufanya usajili jambo lililokua linachukua muda mwingi sana.
 Baadhi ya wanafunzi wapya wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipatiwa huduma za kuweka na kutoa fedha kutoka Benki ya CRDB kupitia matawi yake yanayotembea na wakala wa benki (FahariHuduma), ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
 Wakala wa FahariHuduma wa Benki ya CRDB akichukua taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wakatika walipowasogezea huduma za kuweka na kutoa fedha ili kurahisisha malipo mbalimbali yanayofanywa na wanafunzi wakati wanajisajili chuoni ikiwemo kulipia ada na gharama nyingine za chuo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma wakiendelea kupatiwa huduma kutoka kwa Maafisa wa Benki ya CRDB wa tawi lake linalotembea na wakala wa benki (FahariHuduma),

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad