HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 November 2017

AZAM FC YAWAKARIBISHA YANGA NA SIMBA CHAMAZI, YAZIONYA YATAKA MASHABIKI KUWA WASTAARABU

Afisa Wa Habari wa Azam Fc Jaffer Idd akizungunza na wanahabari.


Uongozi wa klabu ya Azam umewaonya mashabiki wa timu za Yanga na Simba kuwa wastaarabu na vifaa vya uwanja wao katika mechi zao za wikiendi ijayo.

Simba na Yanga zitatumia uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao wikiendi ijayo baada ya uwanja wa Uhuru ambao utakuwa na shughuli za kijamii katika siku hizo.

Afisa habari wa Azam , Jaffer Idd amesema wamefurahi kusikia miamba hiyo itacheza katika uwanja huo lakini wameonya mashabiki kuhakikisha hawaharibu miundo mbinu ya uwanja huo.

"Simba na Yanga zina mashabiki wengi tunawakataka kujitokeza kwa wingi lakini kikubwa wasiharibu miundo mbinu ya uwanja wetu," alisema Jaffer.

Simba ndio itakuwa ya kwanza kutumia uwanja huo siku ya Jumamosi itakapo ikaribisha Lipuli wakati Yanga ikicheza na Prisons siku ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad