HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2017

ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU

Askofu “Atallah Hanna’ ambae ni Askofu Mkuu wa Sebastia wa Kanisa la Orthodox la Kigiriki, amesema: "Uwepo wa Ukristo katika nchi hii takatifu (Palestina), ni uwepo wenye historia ya tangu, kwani Ukristo haukuja Palestina kutoka mahali popote duniani, bali umesambaa kutokea hapa katika ardhi takatifu aliyoichagua Mungu,ili iwe ni sehemu ya upendo wake kwa wanadamu".
Askofu “Hanna”ameongeza kusema kuwa, "Tunatoa wito kwa watoto wetu wasome historia ya kanisa lao na waelewe urithi wao wa kiimani, kibinadamu, kiroho na kiuzalendo. Haifai kuwa hawaelewi historia na mizizi yao ya kina (asili yao) iliyo katika udongo wa nchi hii takatifu. Tunaamini kanisa moja ambalo ni chuo kikuu kitakatifu cha kiutume, lakini pia tunajivunia kuwa sisi ni wana wa nchi takatifu ya Palestina. Tunajivunia kuwa sisi ni wa nchi hii, historia yake, urithi wake na utambulisho wake, huku tukitetea haki ya masuala ya wananchi wake."
Aidha amesema "Katika kumbukumbu ya azimio baya la Balfour, upendeleo wetu utabaki daima na wananchi wa Palestina na kwamba kuvamiwa Palestina kumetokana na azimio la Balfour na wala hakukutokana na Mungu. Hatuwezi kuwakubalia wale wanaomnasibisha Mungu na jambo ambalo sio lake, wala kuwakubalia wale wanaofasiri Biblia kama wapendavyo, hatimae wakasema na kuhalalisha alichokiharamisha Mungu.” 
“Tunaamini kwamba Mungu hakuhalalisha mauaji, vurugu, kuhamisha watu kwa nguvu na matendo ya kukiuka Utu na hadhi ya kibinadamu, tunaamini kwamba maadili haya yapo katika dini tatu za kumpwekesha Mungu. Katika imani yetu ya kikristo na kwa mujibu wa maadili yetu ya kiinjili, tunasema haifai kudhulumiwa au kukandamizwa binadamu yeyote, yale yaliyotokea mwaka 1948 ya kuwatoa kwa mabavu Wapalestina katika makazi yao, miji yao na ardhi yao takatifu, sio haki kwa njia yoyote.”
“Yanayofanywa na baadhi ya makundi ya kiimani ya kizayuni nchini Marekani na sehemu nyingine ambayo yanalihusisha tukio la mwaka 48 na dini, tunawaambia kwamba kilicholitokea taifa letu hakipo hivyo kwa njia yoyote, tunapinga mtu kututafsiria Biblia kwa njia isiyofaa na kwa kuzingatia athari za kizayuni. Hawa wanaharibu maadili na ujumbe wa Kikristo katika ulimwengu wetu huu, ambavyo vimekuwa na daima vitaendelea kuwa ni ujumbe wa upendo, undugu, amani na upendeleo wa wenye kudhulumiwa na wenye kuteswa katika dunia hii.”
Askofu “Atallah Hanna’ ameongeza kusema kwamba "Sisi kama Wakristo na Waislamu kwa pamoja tunaitetea Jerusalemu, sehemu zake takatifu na wakfu zake,huku tukiomba zifeli njama zote dhidi yetu bila kumbagua yeyote kati yetu.
Askofu ameyasema hayo asubuhi ya siku ya Novemba 2, alipokuwa akipokea ujumbe wa kikristo kutoka eneo la “Acre” upande wa kaskazini, uliotembelea Kanisa la Ufufuo na kukutana nae. Ujumbe huo umeelezea heshima na shukrani zao kwa uwepo wa Askofu na utetezi wake kwa Jerusalemu, sehemu zake takatifu na wakfu zake, vilevile utetezi wa kudumu wa Askofu katika uwepo wa kikristo kwenye kitongoji hiki takatifu  duniani.”
Aidha, katika mapokezi hayo pia yalijadiliwa mambo kadhaa likiwemo  suala la Jerusalemu na vilivyomo pia uwepo wa kikristo katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad