HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 18 October 2017

WAZIRI KALEMANI AKUTANA NA MABALOZI WA UJERUMANI, DENMARK NA PAKISTAN

Leo tarehe 18 Oktoba, 2017 Waziri wa Nishati, Dkt.  Medard Kalemani amekutana na mabalozi kutoka katika nchi za Ujerumani, Denmark na Pakistan katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao lilikuwa ni kujadili  ujenzi   wa kiwanda cha mbolea katika mikoa  ya Lindi na Mtwara. Mradi huo unatekelezwa na kampuni za Helm na Ferrostaal za nchini Ujerumani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Ujerumani Nchini, Dkt. Detlef Waechter.
Kutoka kulia Balozi wa Ujerumani Nchini,  Dkt. Detlef Waechter, Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen, Balozi wa Pakistan Nchini, Amir Khan na Mtendaji kutoka Kampuni ya Ferrostaal Topsoe ya Ujerumani, wakifuatilia maelezo  yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati, Dkt.  Medard Kalemani (hayupo pichani)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa kwanza kushoto mbele) na watendaji wengine wa Wizara wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Balozi wa Denmark Nchini, Einar Jensen (hayupo pichani.)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad