HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 11, 2017

WATANZANIA WATAKIWA KUMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUTUMIA MAPINDUZI YA VIWANDA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kufanya nchi hii kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuendelea kusimamia mawazo wa aliyekuwa Rais wa kwanza nchini Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, William Tata Ole Nasha alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius .K. Nyerere lilifanyika katika ukumbi wa Utamaduni wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mtazamo wake wa kuanzisha ,kuendeleza na kudumisha viwanda vya ndani ya nchi kukidhi mahitaji ya wananchi pasipo kutegemea Zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi .uthubutu wa kuanzisha Viwanda vya nguo kama vile Kiwanda cha Urafiki ,Mwatex , Mbeyatex na Mutex ni hatua inayokisi mtazamo wake juu ya Viwanda.” Amesema Ole Nasha.

Amesema hivyo kwa namna ya pekee nimpongeze Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavyosimamia utekelezaji wa mpango huu kwanza kwa kurejesha maadili kwa viongozi na kusimamia matumizi ya rasilimali bora za nchi.

Kwa upande wake mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Prof. Shadrack Mwakalila amesema Baba wa Taifa alisema Julai 29 mwaka 1961 wakati wa ufunguzi wa chuo hicho kuwa alisema kuwa wale wote watakaopata nafasi ya kusoma na kufuzu kivukoni watafanana ma hamira katika mkate. Haiwezekani kutenga hamira katika mkate bali tunajua hamira ipo kwa kutazama jinsi ilivyomua mkate.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , William Ole Nasha akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof Mark Mwandosya akizungumza wakati wa Kongamano la la mahadhimsho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kongamano la Mahadhimisho ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mama Anna Makinda akizungumza wakati akifungua mdahaloi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni , Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa kutoa neno la ukaribisho wa wajumbe waliofika katika kongamano la Maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Kaimu Balozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini akikabidhi zawadi ya Vitabu zinavyomzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kongamano la Maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Sehemu ya Wajumbe walio hudhulia Kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Mkurugenzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere , Joseph Butiku akizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano kizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wajumbe walioshiriki kwenye Kongamano la Mahadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa utamaduni wa Chuo cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad