HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 9, 2017

WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
 
Watu watatu, mchimba makaburi Mohammed Maganga (61)  Khalid Mwinyi (33), anayedaiwa kuwa meneja Wa benki na mfanyabiashara Rahma Almas maarufu baby (37)    wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibi tuhuma za mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52).

Washtakiwa hao wamesomewa shtaka la mauaji.

Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali Adolf Mkini akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amedai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 16 mwaka huu katika makutano ya barabara ya Chole na Haike Selasie Kinondoni Dar es salaam, ambapo wote kwa pamoja wanadaiwa kumuua Lotter.

Baada ya kusomewa kosa hilo la mauaji, Hakimu Mashauri alisema kosa hilo halina dhamana kesi hiyo ikaahirishwa hadi  Oktoba 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, Maganga, Rahma Mwinyi na mwanafunzi Alma's Sued wamesomewa shtaka lingine la uhujumu uchumi na kukutwa na Bomu la kurusha kwa mkono.

Mbele ya Hakimu Mashauri wa mahakam hiyo, Imedaiwa kuwa,Septemba 16 mwaka huu, watuhimiwa hao wakiwa eneo la Upanga DSM walikutwa na silaha moja aina ya Uzigun bila kibali.

Aidha imedaiwa kati ya September 16 mwaka huu washtakiwa hao walikutwa na risasi 167 bila kibali, vilevile  wanadaiwa kukutwa na Bomu la kurusha kwa mkono (Hand grenade) bila kibali.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo, huku upande wa mashtaka ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili wa utetezi Mluge Karoli aliomba dhamana kwa washtakiwa kwani shtaka hilo linadhamana,

Akiwasomea masharti ya dhamana, hakimu Mashauri aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini 2 watakaosaini bondi ya milioni 20 kila mmoja.

Hata hivyo, ni mshtakiwa Swedi tu ndio aliweza kutimiza masharti ya dhamana huku washtakiwa wengine wakishindwa kutimiza masharti, kesi imeahirishwa hadi October 23 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad