HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 4, 2017

WAAFUNZI WAASWA KUHUSIANA NA SOKO LA AJIRA.

ILI kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo. 

Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

"Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 

Mgeni rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule 37 za sekondari za halmashauri ya mji huo. 

Mwandila alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani, anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu, madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha ya kusoma kwa bidii zaidi. 

Aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu, kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza elimu ya sekondari mwakani. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134. 

Gaitu alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016. 

Alisema wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati. 
Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad