HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 18, 2017

VITAMBULISHO VYA TAIFA VYAKUSANYA MAELFU YA WANANCHI WA KATA MASAMA MASHARIKI WILAYA YA HAI –KILIMANJARO

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro limechukua sura mpya baada ya wananchi kuendelea kuhamasika na kufurika kwa wingi kwenye vituo vya Usajili kujisajili.
wananchi wa Kata ya Masama Mashariki Wilaya ya Hai ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa katika kituo cha Usajili kilichopo kwenye kijiji cha Mbweera, Mboreny, Sonu, Ngira na Sawe. Zoezi katika Kata hiyo litamalizika Jumatano 18/10/2017 kabla ya kuhamia Kata za Masama Magharibi na Kata ya Kia. 
Zoezi la Usajili kwa mkoa wa Kilimanjaro linaendelea katika Wilaya zote za mkoa huo ikiwemo Moshi, Rombo, Siha, Mwanga na Same.
 Mmoja wa Wakazi wa Kijiji Mbweera Kata ya Masama Bi Rachel akiweka saini ya kielekektroniki kwenye mashine ya kuchukua taarifa wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Kata hiyo.
 Afisa Usajili Wilaya ya Hai Bw. Abubakar Karinga akitoa maelekezo ya taratibu za Usajili kwa wananchi waliokusanyika kusajiliwa kutoka vijiji vya Mbweera na Mboreny.
  Wananchi wa Kata ya Masama wakiendelea na hatua za Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hili likiendelea, ambapo mbali ya na kujaza fomu za maombi pia wanachukuliwa alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki. 
 Wananchi wa Kata ya Masama wakiendelea na hatua za Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hili likiendelea, ambapo mbali ya na kujaza fomu za maombi pia wanachukuliwa alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki. 
Bi. Anocensia Momburi mmoja wa Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitabasamu jambo wakati akimhudumia mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mbweera aliyefika kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad