HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 27 October 2017

VIONGOZI WA WALEMAVU AFRIKA WAJADILI SERA YA PAMOJA KWA WALEMAVU

Mwenyekiti wa Shirikiso la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania(SHIVYAWATA), Ummy Ndeliananga akizungumza katika mkutano wa siku mbili ambapo watazungumza masuala mbalimbali ya walemavu katika nyanja mbalimbali kama kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza katika nchi zote za afrika.
 
VIOGOZI wa vyama vya walemavu barani Afrika wakutana jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujadili maswala mbalimbali ya walemavu pamoja na kuwa na sera ya pamoja ya walemavu barani Afrika.

Maswala na sera wanazozijadili ni pamoja na maswala ya
kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ambapo yatawapa fursa walemavu kujikwamua  kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirikiso la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Ndeliananga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa bara la Afrika unaoendelea kufanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.

Tunatakiwa kuwa na sauti ya pamoja watu wenye ulemavu barani Afrika ambapo tutakuwa na hatua tofautitofauti pia ametoa wito kwa serikali kujenga miundombinu ambayo inafikika kwa walemavu wote katika bara la Afrika.
  Mkurugenzi wa mipango  na ushirikiano wa kimataifa wa Africa Disability alliance), Mpho Ndebele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Muungano wa watu wenye ulemavu wa nchi za bara la Afrika ili kuwa na sera ya pamoja katika kila nchi ili kuwapa nafasi wa lemavu katika nyanja mbalimbali kama kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza.
 Watafsiri wa Lugha za Alama kutoka Kenya na Uganda wakitafsiri mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ya kuunda sera ya pamoja ya walemavu wa bara Afrika.
 Mtafsiri wa lugha za Alama kulia azingumza na watu wenye ulemavua ambao ni viziwi ili kwenda pamoja katika mkutano utakao fanyika kwa siku mbili ambapo walemavu watajadiliana masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kimiundombinu, kijamii, kiafya, ajira na kielimu ili kupata sauti ya pamoja katika nchi za bara nzima bila kuangalia ni nani anaongoza.
 Mkurugenzi mtendaji wa Muungano wa walemavu Afrika kutoka nchini Afrika Kusini (Africa Disability alliance), Dagnachew Wakene akizungumza wa viongozi mbalimbali wavyama vya walemavu barani Afrika wakizungumza maswala mbalimbali ya walemavu na kuunda  sera ya pamoja kwa bara la Afrika.
 Mratibu wa Mkutano wa viongozi wa watu wenye ulemavu, Oktaviani Simba akizungumza katika mkutano unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu barani afrika wakiwa katika mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad