HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 October 2017

UWT MKOA WA MBEYA WATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI KUELEKEA MAHADHIMISHO YA MIAKA 38

Na Mwandishi wa Globu ya Jamii Mbeya

Umoja wa wanawake wa  Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Mbeya mjini  imendesha zoezi la kutoa elimu ya afya ya uzazi na Maendeleo  kwa wanafunzi  wa shule ya kutwa ya Mbeya .

akizungumza na Globu ya Jamii   Katibu wa UWT  Mkoa wa Mbeya , Mary Mwenisongole amesema kuwa kwa kushirikiana na wataalam wa afya na Maendeleo ya jamii,leo tarehe  wameshiriki kutoa elimu ya afya na kujitambua kwa watoto wa kike zaidi ya 500 shule ya sekondari ya kutwa Mbeya ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya wiki ya  miaka 39 ya jumuiya ya wanawake.

'' Sisi kama Jumuiya ya Wanawake wa chama kikongwe hapa nchini tumeona kuwa katika shamra shamra za miaka zaidi ya 38 ya Jumuiya yetu ndani ya chama ni vyema tukaanza kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike waliopo mashuleni kwani wao ndio Viongozi wa UWT ya baadae" amesema .

  Akishukuru kwa niaba ya ya Walimu mwalimu wa nidhamu   Benson John aliishukuru jumuiya kwa jambo walilofanya na kuomba waendelee kwani tatizo la mimba ni kubwa na kwa mwaka huu 2017 kufikia mwezi wa 9 wanafunz 6 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na tatizo la ujauzito.

 UWT  mkoa wa Mbeya imewahakikishia walimu kuwa zoezi hili lita kuwa endelea na katibu UWT ameahidi kufika mara nyingi iwezekanavyo kupitia mpango  wa sauti ya shangazi ambayo imepokelewa kwa shangwe, na wanafunzi wameahidi kutoa ushirikiano kwa SHANGAZI.

 Katibu wa UWT mkoa wa Mbeya Mary Mwenisongole   akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya katika programu ya Ongea na Shangazi
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mbeya Mjini Mama Mtani akizungumza na na Wanafunzi wa kike wa Mbeya kutwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad