Mwenyekiti wa mtaa wa akimsaidia kujaza
fomu ya kitambulisho cha Taifa mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa
katika zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Usajili Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya umeanza katika Kata za Matema, Makwale, Mababu na Ndobo na unatarajiwa kumalizika Jumamosi Octoba 14, 2017 na kuendelea Kata zingine.
Kwa mujibu wa msimamzi wa zoezi hilo Kanda ya Mbeya ndugu Magohu Zonzo amesema mwitiko mkubwa wa wananchi unatoa imani ya zoezi hilo kumalizika ndani ya siku zilizopangwa na kutoa fursa kwa Kata zingine kusajiliwa.
Ameeleza faida za Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa watu kwa Taifa na namna kila mwananchi atakavyonufaika na mfumo huo utakapoanza kutumika na hivyo kutoa wito kwa jamii hususani wananchi wa Wilaya ya Kyela kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kusajiliwa.
Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeanza kwa kishindo mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini na linakusudiwa kumalizika ndani ya muda mfupi kutoa fursa kwa mikao mingine ya Tanzania kusajiliwa.
Mmoja wa wakaazi wa Mbeya akiweka saini ya
kielektroniki wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea
wilayani Kyela.
Baadhi ya wananchi wakisubiri kusajiliwa
wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wilayani Kyela, wakati
wengine wakiendelea Kusajiliwa na Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa wakati zoezi linaendelea.
Wakazi wa kijiji cha Kisyosyo Kata ya Matema wilayani Kyela mkoa wa Mbeya wakichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment