Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma wa Kampuni ya simu ya Tigo, David Umoh (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Uzoefu wa Wateja wa Kampuni ya simu ya Tigo, Sarah Cyprian.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na
uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha
wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa
salaam.
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo
Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia
wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka.
Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00#
itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua
rahisi zaidi. Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na
muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la
menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya
fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya
ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara
watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.
Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja
kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za
matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake.
‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya
kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na
uliosambaa kote nchini,’ alisema.
Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji
ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu
za mkononi nchini. Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti
na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia
ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya
miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya
fedha ya nchi husika.
‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya
kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia
Watanzania. Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia
mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema.
Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza
kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao
wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa
urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment