HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 7 October 2017

TECNO YAJA NA DUKA JIPYA LA SMART HUB MLIMANI CITY.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Kampuni ya kuuza Simu za Mkononi ya TECNO imeeendelea kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora Zaidi kuwahi kutokea katika biashara simu kwa kutengeneza duka jipya la kisasa zaidi linalokwenda kwa jina la TECNO SMART HUB.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni afisa Mauzo Mtandaoni Erick Daniel amesema kuwa duka hili jipya la kisasa linatarajiwa kufunguliwa eneo la Mlimani city , jengo jipya ambapo kutakua na watu maarufu mbalimbali walioalikwa , wadau wa kampuni ya TECNO pamoja na mashabiki wa TECNO mitandaoni. 

"Duka hili kubwa linalotarajiwa kufunguliwa siku ya jumamosi maaraufu kama TECNO SMART HUB litakua linatoa huduma bora zadi ya maduka mengine ya kawaida ya simu. Huduma zinazotarajiwa kutolewa katika TECNO SMART HUB ni pamoja na mauzo, huduma baada ya mauzo na kikubwa katika maduka haya elimu mahsusi juu ya matumizi ya simu janja “smartphone” itakua inatolewa na wabobezi wa simu hizo watakao kua dukani muda wote, lakini pia wateja watkaohudumiwa katika duka hili wataapta nasafi ya kupumzika na kupata vivywaji huku wakipata huduma bora".

Amesema TECNO SMART HUB itazinduliwa siku ya jumamosi tarehe 7 ambapo watu 200 wa kwanza kuingia dukani watapata zawadi za bure wakati kwa wanunuaji wa simu siku hiyo watakua na nafasi za kupata zawadi mbili kwa mpigo, furaha Zaidi ni pale ambapo wateja wote wataweza kuingia katika bahati nasibu ya kushinda televishen ya inchi 32 mbili pamoja na zawadi zingine kama feni, power bank na majagi ya umeme. 

Wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya, vinywaji baridi vitakua vinatolewa kwa wateja wa bidhaa mbalimbali zikiwemo hata vifaa vya simu pamoja na siu zenyewe, kadi maalumu za matengenezo ya simu zitatolewa pia kwa wateja “VIP card”, huku burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali zikitawala eneo hilo kuhakikisha TECNO SMARH HUB linakua sehemu ya kisasa Zaidi. 

TECNO inawaalika wateja wote kwenda kununua simu kattika duka hili jipya la kisasa ili kujishindia zawadi mbalimbali na kuingia katika familia ya TECNO kupitia bidhaa zilizopo katika SMART HUB. 
Baadhi ya wafanyakazi kampuni ya simu za mkononi wa Tecno wakiwa katika mitaa ya Kariakoo wakiwa katika maandamano ya kutangaza bidhaa hizo
Baadhi ya wafanyakazi kampuni ya simu za mkononi wa Tecno wakiwa katika mitaa ya Kariakoo wakiwa katika maandamano ya kutangaza bidhaa hizo
Baadhi ya wafanyakazi kampuni ya simu za mkononi wa Tecno wakiwa katika mitaa ya Kariakoo wakiwa katika maandamano ya kutangaza bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad