HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 25, 2017

Tamasha la magari kufanyika Oktoba 27 viwanja vya The Kenyatta Drive

 Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga (katikati) akieleza jambo juu ya Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Bw. Oscar Ruhasha. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu.  
 Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd,  Aluwy Amar ambao ni wadhamini wa Tamasha la Magari Tanzania akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu bidhaa mbalimbali watakazokuwa nazo katika tamasha hilo leo jijini Dar es salaam. Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga. Kushoto ni Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group Bw. Abdul Wahab. Tamasha hilo litafanyika kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay.
Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group, Abdul Wahab akieleza jambo juu ya Tamasha la Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu.
(Picha na Thobias Robert- Maelezo) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad